Mavazi yatokanayo na magamba ya miti yamerudi kwenye fasheni nchini Burundi kutokana na ubunifu waa shirika la Murundi Fashion. Shirika hilo lililoundwa na msichana Kabatesi Anick limekuwa likitengeneza nguo hizo katika mitindo ya kisasa likidhamiria kufufua na kutambulisha utamaduni wa kale wa nguo za miti Burundi. Amida Issa anaangazia kazi ya shirika hilo katika makala ya Utamaduni na Sanaa.