Ucahguzi wa bunge na madiwani haukuwa wa haki na huru
3 Julai 2015Matangazo
Uchaguzi huo uliogubikwa na vurugu na kususiwa na baadhi ya vyama vya upinzani ulifanyika licha ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuitolea mwito serikali ya Burundi kuahirisha uchaguzi huo kufuatia hali mbaya ya kiusalama. Hata hivyo hadi leo raia wa nchi hiyo wanaendelea kusubiria kwa hamu kubwa matokeo hayo yaliokuwa yatolewe rasmi hapo jana. Kwa mengi zaidi juu ya hilo, Amina Abubakar amezungumza na mwandishi wetu Amida Issa aliyeko mjini Bujumbura .
Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri:Yusuf Saumu