Mzozo wa kidiplomasia kati ya Burundi na jirani yake Rwanda umepata sura mpya, baada ya msemaji wa chama tawala nchini Burundi cha CNDD/FDD- Gerase Daniel Ndabirabe, kutoa tangazo kupitia redio ya taifa akimshutumu vikali rais wa Rwanda Paul Kagame kuwa ni chanzo cha matatizo ya Burundi.