Julai mosi, ni siku ambayo Burundi inaadhimisha miaka 58 tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa mkoloni Ubelgiji. Akilihutubia taifa, rais mpya Evariste Ndayishimiye ametanganza kuwa virusi vya corona ni janga na kuahidi kukabiliana nalo. Pia ameahidi kufanya majadiliano na watu walioikimbia nchi, kurejesha marupurupu ya kila mwaka kwenye mishahara ya wafanyakazi wa serikali.