AfyaCameroon
Cameroon yaweka vizuizi mkapani na Guinea ya Ikweta
10 Februari 2023Matangazo
Hatua hiyo imejiri baada ya kutokea vifo kadhaa ambavyo kiini chake bado hakijafahamika, vikihusishwa na aina fulani ya homa.
Taarifa ya wizara ya afya ya taifa hilo inasema vizuizi hivyo vina lengo la kuchunguza kiwango cha hatari kwa ugonjwa huo kwa lengo la kubaini na kushughulikia kisa chochote katika hatua ya mapema.
Uchunguzi unaendelea na ufuatiliaji umeimarishwa kwa ushirikiano wa wajuzi kutoka shirika la Afya Duniani pamoja na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Atlanta.
Wizara ya afya ya Cameroon ilitoa taarifa jana Alhamis ikisema imerekodi karibu vifo 20 katika vijiji vya jimbio la Kie-Ntem huko Guinea ya Ikweta ambavyo vinapakana na Cameroon.