CARACAS:Venezuela kuziepuka IMF na benki ya Dunia
1 Mei 2007Matangazo
Rais Hugo Chavez wa Venezuela amesema nchi yake itajiondoa kwenye mashirika ya kutoa mikopo ya fedha ya IMF na Benki kuu ya dunia.
Chavez ambaye anataka kuifanya Venezuela kuwa nchi ya ujamaa amesema mashirika hayo yenye makao yake makuu Washington Marekani yanapasa kulaumiwa kwa kuendelea kusababisha umaskini katika nchi Amerika ya Kusini.
Chavez anapanga kuunda shirika mbadala ambalo litakuwa mkopeshaji wa nchi hizo na litakalosimamiwa na mataifa ya eneo hilo.