CDC:Matumaini ya kufikishwa chanjo ya Mpox, barani Afrika
16 Februari 2023Kaimu mkurugenzi wa CDC Ahmed Ogwell amewaambia waandishi wa habari hii leo kwamba dozi hizo za Mpox zitapelekwa kwanza kwenye mataifa yenye mahitaji makubwa. Congo na Nigeria ni miongoni mwa mataifa hayo.
Julai mwaka jana, shirika la afya ulimwenguni, WHO liliyataja maradhi hayo kuwa dharura ya kimataifa wakati kukishuhudiwa mlipuko barani Ulaya na Amerika Kaskazini, na kisha kuiomba jamii ya kimataifa kuisaidia Afrika.
Soma pia:Visa vya homa ya nyani vyaongezeka mara tatu barani Ulaya
Hata hivyo hakukua na taifa lililojitokeza kusaidia chanjo wala matibabu hata kuliposhuhudiwa ongezeko la maambukizi.
Tangu mwaka 2000, Afrika imeripoti karibu visa 1,000 hadi 2,000 vinavyodhaniwa kuwa vya homa ya nyani kila mwaka, lakini mwaka jana kuliripotiwa visa zaidi ya 3,000.