SiasaChad
Chad yafanya kura ya maoni kuamua kuhusu rasimu ya katiba
17 Desemba 2023Matangazo
Vituo vya kupigia kura tayari vimefunguliwa tangu mapema asubuhi na vitafungwa mnamo saa kumi na moja jioni kwa saa za nchi hiyo.
Utawala wa kijeshi ambao ulichukua madaraka mnamo 2021 umesema kura hiyo ya maoni ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi mkuu unaopangwa kufanyika mwakani ili kuirejesha Chad chini ya utawala wa kiraia.
Sehemu kubwa ya upande wa upinzani na makundi kadhaa ya kiraia yametoa mwito wa kususiwa kura hiyo ya leo.
Wanasema iwapo katiba hiyo itaidhinishwa, itafungua njia ya kuchaguliwa kwa rais wa mpito Mahamat Idriss Deby Itno na kurefusha utawala wa familia yake ulioanza miaka 33 iliyopita pale ya baba yake hayati Idriss Deby alipotwaa madaraka kwa njia ya mapinduzi.