Chama cha Democratic huko Albania kimeshinda uchaguzi wa bunge
6 Julai 2005Matangazo
Baada ya kutangazwa sehemu ya matokeo ya uchaguzi wa bunge uliofanywa Albania, chama cha Democratic cha rais wa zamani, Sali Berisha kimeshinda. Lakini kimeshindwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura. Hata hivyo, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, chama cha Democratic kimeshinda moja kwa moja viti 55 kati ya 100 vya bunge. Chama cha kijamaa cha Fatos Nano kimepata viti 42. Viti viliobakia vimechukuliwa na vyama vitatu vidogo. Chama cha Democratic kimeshatangaza kwamba kinataka kuunda serekali ya mseto na Chama cha Republican. Matokeo yamwisho yanatarajiwa kutangazwa baadae leo.