Chama cha FDP chayumba kuhusu mafao ya familia
26 Septemba 2012Gazeti la Frankfurter Rundschau, limeandika kuhusu fedha zinazolipwa na serikali kwa familia zenye watoto. Gazeti linaandika.
Ukiangalia kwa undani chama cha FDP kinashangaza. Kinajionyesha kuwa kama chama chenye msimamo, chama kisichotaka kushiriki katika kila kitu, lakini kinataka kubakia madarakani, chama ambacho kinatoa ishara kupinga mchanganyiko wa nadharia na pia matumizi mabaya. Hii ilikuwa siku ya Jumatatu, mhariri anasema kuwa uongozi wa FDP ulipopinga suala hili la mafao ya familia. Je Philipp Rösler kiongozi wa chama hiki anatambua kinachotokea? Hilo lilikuwa kosa. Siku ya Jumanne FDP imeonyesha sura nyingine na kuunga mkono mpango huo wa mafao ya familia. Hii inawezekana kuwa ni mchezo wa ukiwatunukia wateja wako zawadi , nami pia nitawapa wangu.
Kuhusu mada hiyo hiyo , gazeti la Hamburger Abendblatt , linaandika:
Kelele za FDP dhidi ya muafaka kuhusu mafao ya familia yana lengo lake. Chama hicho cha kiliberali , hakielekei kufanya mabadiliko yake ya ndani kuhusu hatua walizozichukua ambazo hazipendelewi na wapiga kura , na wala hawana nia kamili ya kujionyesha kuwa wana lengo la kuonyesha msimamo wa kisiasa katika masuala ya familia. FDP inataka tu kuangalia ukweli. Kinajiona baada ya kuwa sawa kisiasa na vyama vingine vinavyounda serikali ya mseto katika muda wa miaka mitatu sasa kuwa kinazidi kutupwa kando.
Kama alivyosema kiongozi wa FDP , Rösler wakati akiingia madarakani Mei mwaka 2011 kuwa anataka chama hicho kufikia malengo yake. Pamoja na hayo kuna hatari chama hicho kikaangukia pua katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika katika miezi 12 ijayo. Katika hilo binafsi kansela Merkel hataki kuliangalia. Kimsingi anataka Merkel kufanyakazi na Rösler katika serikali mpya baada ya uchaguzi. Kwa hiyo ni lazima Merkel achukue hatua hizi sasa ya kuiokoa FDP.
Rais wa Marekani Barack Obama alihutubia hadhara kuu la umoja wa mataifa mjini New York. Kuhusu yale aliyoyazungumza , wahariri pia wameyatafakari. Hii hapa ni tafakuri ya mhariri wa gazeti la Badische Zeitung.
Barack Obama anakabiliwa na uchaguzi, anaanza kuandika mhariri. Kwa hiyo alitaka kuzungumzia japo kidogo kuhusu kiini cha matatizo yanayozungusha vichwa ya mizozo mikubwa na maeneo ambayo yanakabiliwa kila mara na matatizo. Katika suala hili huenda , kuwa mkweli na wazi ni jambo linaloweza kusaidia, kwa ajili ya yeye kuchaguliwa tena , lakini huenda pia ni hatari. Obama amejaribu kuepuka , lakini hata hivyo mtu hawezi kumtupia lawama kwa hilo.Kwa mfano katika hali ya Syria ama mvutano wa kinuklia na Iran , nchi zenye nguvu kama China na Urusi huingilia na kuzuwia. Wito wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon , kwa baraza la usalama kuchukua hatua za haraka katika suala la Syria , umekuja umechelewa mno. Lakini anasikika kama amekata tamaa.
Mada nyingine iliyopewa umuhimu na wahariri ni kuhusu mfumo wa mafao ya uzeeni. Gazeti la Bild linaandika.
Jana (25.09.2012) haikuwa siku nzuri kwa chama cha SPD. Uongozi wa chama cha SPD ulikabiliwa na mbinyo mkali kutoka kwa vyama vya mrengo wa shoto na vyama vya wafanyakazi kushinikiza kuachana na mpango wake wa wafanyakazi kustaafu wakiwa na umri wa miaka 67. Hali hiyo ilikuwa mbaya. Lakini inaweza kuwa mbaya zaidi.
Iwapo SPD hadi mwishoni mwa mwezi Novemba itapunguza kiwango chake cha mafao ya uzeeni kutoka asilimia 43 hadi ifikapo mwaka 2030, chama hicho kitapoteza uaminifu wake kuwa chama kinachojali maslahi ya jamii kwa wapiga kura wao.Kwa kuwa jamii inazidi kuwa na wazee wengi, hakuna jibu litakalokubaliwa , isipokuwa kuongeza fedha zaidi katika kapu la mafao ya uzeeni.
Nalo gazeti la Frankfurter Neue Presse likiandika kuhusu mada hiyo linasema:
Mpango wa mafao ya uzeeni wa kiongozi wa chama cha SPD ni ishara mambo yanayokuja hapo baadaye, utawala wa hapo baadaye utakaoundwa na vyama vya SPD na CDU, kama baadhi ya watu wanavyotabiri. Kama mpango wa euro 850 wa waziri wa jamii Ursula von der Leyens wa nyongeza ya ziada kwa ajili ya mafao ya uzeeni. Katika wakati ambapo Ujerumani imetumia mabilioni ya euro kuyaokoa mataifa yaliyo katika madeni , raia kila hawafahamu , ni kwa nini michango yao ya mafao ya uzeeni na kodi yao haiingia katika kuwasaidia .
Na hadi hapo ndio tunafikia mwisho wa kuwaletea yale yaliyoandikwa na wahariri wa magazeti ya hapa Ujerumani. Aliyewakusainyia mara hii ni Sekione Kitojo.
Mwandishi : Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman