SiasaAsia
Chama cha Imran Khan chapata mwenyekiti mpya
2 Desemba 2023Matangazo
Hatua ambayo inakipa nafasi chama cha Khan kushiriki katika uchaguzi ambao umepangwa kufanyika Februari mwakani.Mwanasheria Barrister alikuwa ameteuliwakuwa mwenyekiti wa Pakistan Tehreek-e-Insaaf (PTI), na Khan mwenyewe aliye gerezani na kuzuiwa kushiriki uchaguzi.Tume ya Uchaguzi ya Pakistan ilikuwa imeagiza PTI ifanye uchaguzi wa mwenyekiti wake mpya ikiwa kingetaka kushiriki uchaguzi wa mkuu wa Februari 8.Chama cha PTI kitakabiliana na upinzani mkubwa kutoka katika chama cha waziri mkuu wa zamani Nawaz Sharif. Lakini wakili aliyechaguliwa Jumamosi hii hatolazimika kuwa waziri mkuu, endapo chama chake kitashinda.