1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Kijani Ujerumani chataka mazungumzo rasmi

6 Oktoba 2021

Chama cha Kijani kinatetea ulinzi wa mazingira kimesema kinataka kuanza mazungumzo rasmi na chama cha Social Democratic, SPD na kile cha kiliberali FDP ya kuunda serikali ya muungano utakaovihusisha vyama vitatu.

https://p.dw.com/p/41KJu
Deutschland | Parteitag Bündnis90/Die Grünen
Picha: Omer Messinger/Getty Images

Kiongozi wa chama cha Kijani, Annalena Baerbock amewaambiawaandishi habari leo kuwa baada ya mazungumzo ya awali na SPD pamoja na muungano wa vyama vya kihafidhina CDU/CSU, vilivyoshika nafasi ya kwanza na ya pili katika uchaguzi mkuu wa Septemba, wanaamini kuwa suala la kuwa na mazungumzo ya kina lina mantiki.

Chama cha Kijani kimeshika nafasi ya tatu. Katibu Mkuu wa FDP, Volker Wissing alitangaza muhtasari wa hali iliyopo baada ya awamu ya kwanza ya mazungumzo yaliyofanyika jana kati ya muungano wa vyama vya kihafidhina CDU/CSU na Kijani.