Chama cha UDA cha taraji ushawishi mkubwa bungeni Kenya
12 Agosti 2022Disemba mwaka 2020 chama cha UDA kilizinduliwa, na muda mfupi baadaye kikampokea mwanasiasa mkwasi, naibu Rais Wiliam, alipokihama cha tawala cha Jubilee. Ruto amegombea Urais kwa tiketi ya chama hicho, na amezuru kote nchini akikitafutia chama hcha cha UDA umaarufu.
Chama cha UDA kimetwaa viti vingi ya kisiasa kwenye eneo zima la bonde la ufa na mlima Kenya kwenye uchaguzi mkuu. Katika eneo la Nakuru, kati ya wabunge 11, tisa wamechaguliwa kwa tiketi ya UDA. Wagombea wa UDA katika viti vya Gavana, Seneta na Mwakilishi wa wanawake wanaongoza kwenye matokeo ya uchaguzi.
Kando na ushawishi huu mkubwa, baadhi ya wagombeaji wa UDA wamejipata kwenye upande mbaya wa sheria katika kipindi cha uchaguzi huu mkuu.
Ushawishi bila maadili ?
Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria ambaye alikuwa akikitetea kiti chake alikamatwa siku ya uchaguzi kwa tuhuma za kumshambulia na kumsababaishia majeraha mwanasiasa mwenzake kwenye kituo cha kupiga kura. Aliachiliwa kwa dhamana na anatarajiwa kufika mahakamani tarehe 17 mwezi huu kwa kusikizwa kwa kesi yake.
Vilevile mwezi uliopita Gikaria alizuiliwa na maafisa kutoka idara ya upelelezi kuhojiwa kuhusu kuhika kwake na genge la kihalifu la Confirm ambalo wakati huo lilikuwa linatekeleza mauaji ya watu wasio na hatia. Hata hivyo, licha ya tuhuma hizi, Gikaria ameweza kukitwaa tena kiti chake kama mbunge wa Nakuru Mashariki.
Kisa cha madai ya mauwaji
Huko Bungoma, Mbunge wa Kimilili Didmus Baraza amejisalimisha katika kituo cha polisi kufuatia madai ya mauaji ya msaidizi wa mpinzani wake Brian Khaemba. Idara ya upelelezi nchini ilikuwa imetoa muda wa siku sita kwa Baraza kujitokeza wakisema alitoweka na hajulikani aliko baada Tu ya kumpiga risasi kichwani na kumuua msaidizi huyo siku ya jumanne.
Baraza alikuwa anakitetea kiti chake na alipotangazwa mshindi maafisa wa uchaguzi walikataa kumkabidhi chetu mjumbe aliyemtums aliyemtuma hadi pale atakapokwenda yeye mwenyewe.