1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions League: Ujerumani dhidi ya Uhispania

12 Aprili 2013

Uwezekano wa timu mbili kutoka Ujerumani au timu mbili kutoka Uhispania kukutana mwezi ujao katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Champions League bado uko hai baada ya droo iliyofanywa mjini Nyon Uswisi

https://p.dw.com/p/18F1c
A giant screen displays the draw for the semi-finals of the UEFA Champions League on April 12,2013 at the UEFA headquarters in Nyon. Spanish and German teams were kept apart for the semi-finals of the Champions League, as European football's governing body UEFA made the draw for this year's last four games. AFP PHOTO / FABRICE COFFRINI (Photo credit should read FABRICE COFFRINI/AFP/Getty Images)
UEFA Champions League Auslosung Halbfinale Saison 2012/2013Picha: AFP/Getty Images

Lakini huku timu za Uhispania na Ujerumani zikitenganishwa katika droo hiyo iliyofanywa katika makao makuu ya shirikisho la soka ulaya UEFA ya nusu fainali, fainali hiyo ya uwanja wa Wembley jijini London huenda ikawa pambano jingine la Ujerumani na Uhispania.

Bayern Munich ambao walishindwa katika fainali mwaka jana, na ambao tayari wamenyakua taji la Bundesliga, wanaangushana viongozi wa La liga Uhispania. Katika mchuwano mwingine, Borussia Dortmund watakabana koo na Real Madrid wakati wawakilishi wa miamba ya sasa ya soka barani Ulaya wakiumiza nyasi. Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Aprili 23 na 24, huku za mkondo wa pili zikichezwa Aprili 30 na Mei mosi. Fainali itachezwa jijini London katika uga wa Wembley mnamo Mei 25.

Droo ya Europa League

Katika mechi za Europa League, mabingwa Ulaya Chelsea watacheza dhidi ya Basel huku mchuano wa kwanza ukichezwa nchini Uswisi. Fenerbahce watapambana na Benfica, huku mkondo wa kwanza ukuchezwa Uturuki. Chelsea wanalenga kuwa timu ya nne katika historia kunyakua taji la Champions League na kisha Europa League msimu katika msimu unaofuata. Timu zote nne za nusu fainali zilianza msimu katika ligi ya mabingwa kabla ya kudondoka hadi Ligi ya daraja ya pili. Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Aprili 25 huku za marudiano zikiwa Mei 2. Fainali iztakuwa katika uwanja wa Amsterdam Arena mnamo Mei 15. Na sasa tuangalie Ligi ya soka hapa Ujerumani Bundesliga ambapo kitu kilichosalia tu ni kulinyakuwa taji, na Borussia Dormtund wanaonekana kuchukua nafasi ya pili, na pia vita yva kujikatia tikiti ya moja kwa moja ya ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Timu zote nne za nusu fainali ya Europa League zilianza msimu katika Champions League
Timu zote nne za nusu fainali ya Europa League zilianza msimu katika Champions LeaguePicha: Reuters

Premier League yaidhinisha teknolojia ya Hawk-Eye

Ligi kuu ya soka England imetangaza uamuzi wa kihistoria kuidhinisha matumizi ya teknolojia ya kubainisha mpira umevuka mstari wa lango, kwa msimu wa 2013 – 14 kuendelea mbele. Shirika la Uingereza la Hawk-Eye limechaguliwa kutengeneza teknolojia hiyo ya kisasa katika mkutano uliohudhuriwa na wenyekiti wa vilabu 20 vya Premier League.

Mfumo wa Hawk-Eye hutumia kamera saba kuufwat mpira na kutuma ishara kwa saa za mkononi za maafisa wa mechi katika muda wa sekunde moja kama mpira utavuka moja ya mistari miwili ya langoni. Itawekwa katika viwanja vyote vya Premier League, na Chama cha Soka Uingereza kinanuia kuiweka teknolojia hiyo katika uwanja wa Wembley jijini London ili kutumiwa katika mechi ya kitamaduni ya Ngao ya Jamii mwezi Agosti, inayochezwa kama ishara ya kuufungua msimu mpya wa ligi.

Namna teknolojia ya Hawk-Eye inavyofanya kazi
Namna teknolojia ya Hawk-Eye inavyofanya kaziPicha: Shaun Botterill/Getty Images

Vettel akutana na Webber

Na katika mbio za magari ya Formula One, bingwa wa mara tatu wa ulimwengu Sebastian Vettel hajaonyesha huruma yoyote kwa mwenzake wa Red Bull Mark Webber kuhusiana na mgogoro wa maagizo ya maafisa wa timu, ambao uliugubika ushindi wake wa mashindano ya mkondo wa Malaysian Grand Prix.

Vettel amesema huenda tena akapuuza maagizo ya timu ili kumpita webber, akisema hajawahi kupata uungwaji mkono kutoka kwa Muastralia huyo. Madereva hao wawili wamekutana tena mjini Shanghai kwa mashindano ya kesho Jumapili ya mkondo wa Chinese Grand Prix kwa mara ya kwanza tangu ushindi wa Vettel wenye utata wiki tatu zilizopita. Vettel mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ujerumani amesema mwenzake Webber mwenye umri wa miaka 36 hajawahi kumpa usaidizi. Vettel anasema katika msimu uliopita, katika mashidano ya mkondo wa Brazil, Webber hakumsaidia wakati alipokuwa akipambana na dereva Mbrazil Fernando Alonso wa Ferrari kunyakua taji. Vettel aliomba radhi kwa kikosi baada ya mkondo wa Malaysia lakini akasema hakuelewa ujumbe wa redio ya timu uliomtaka asaliye nyuma ya Webber kwa muda uliokuwa umesalia mbio kukamilika.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP

Mhariri: Mohammed Khelef