Chanjo ya malaria inafanya vizuri Afrika
3 Februari 2024Matangazo
Chanjo hiyo, ambayo tayari ilikuwa imeidhinishwa kutumika na mamlaka za udhibiti katika nchi tatu za Afrika Magharibi na Shirika la Afya Duniani WHO, ni ya pili kuruhusiwa kwa matumizi mwaka huu.Chanjo ya kwanza ilizinduliwa nchini Cameroon mapema mwezi huu ambayo imetengenezwa na kampuni ya GSK.Chanjo zote mbili zina uwezo wa kuzuia maambukizi dhidi ya ugonjwa huo unaoenezwa na mbu ambao bado unaua zaidi ya watu nusu milioni, hasa watotowadogo katika nchi za Afrika katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara kila mwaka.