China na Marekani kuanza tena mazungumzo ya kijeshi
16 Novemba 2023Viongozi hao wawili wamekutana kwa masaa kadhaa pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki, APEC, mjini San Fransisco nchini Marekani.
Xi na Biden waahidi ushirikiano zaidi kati ya mataifa yao
Wawili hao waliahidi ushirikiano utakazozileta karibu China na Marekani katika kurejelea mazungumzo ya kawaida chini ya kile kinachojulikana kama mkataba wa ushauri wa kijeshi wa Bahari ambao hadi mwaka 2020 ulikuwa umetumika kuboresha usalama angani na baharini.
Soma pia: Xi na Biden wawasili San Francisco kwa mazungumzo muhimu
Baada ya mkutano huo kukamilika, afisa mmoja mkuu wa Marekani aliyezungumza kwa sharti la kutotambulishwa, alisema kuwa makubaliano hayo ya kijeshi yanamaansiha kuwa waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin sasa anaweza kukutana na mwenzake wa China pindi atakapochaguliwa.