China na Ufilipino zafikia makubaliano kuhusu eneo la bahari
22 Julai 2024Ufilipino ilipeleka meli ya kivita katika eneo hilo mnamo mwaka wa 1999 ili kuongeza nguvu madai yake. Kundi dogo la wanajeshi wa Ufilipino limepelekwa katika eneo hilo la bahari.
Lakinijeshi la wanamaji la Ufilipino limekabiliana mara kadhaa na meli za ulinzi wa pwani za China wakati zikijaribu kupeleka vifaa na biadhaa na kuwabadilisha mabaharia.
Soma pia:Ufilipino na China zafikia makubaliano kuzima mgogoro
Meli za China zilitumia mizinga ya maji na kuzizuia meli za Ufilipino kufika katika kituo hicho. Sasa, Beijing na Malina zimesema zimefikia maelewano kuhusu suala hilo. Hata hivyo hazikutoa maelezo zaidi kuhusu makubaliano hayo.
China inahusika na mizozo kama hiyo na majirani zake, wakiwemo Brunei, Malaysia, Taiwan na Vietnam. Makabiliano katika Bahari ya Kusini mwa China aghalabu yamechochea hofu ya kuzuka mgogoro mkubwa wa kikanda.