SiasaAsia
China na Urusi zaanza luteka ya pamoja ya kijeshi
17 Julai 2024Matangazo
Gazeti la serikali ya China la Global Times, limesema China na Urusi zitapeleka angalau meli tatu kila moja kwenye mazoezi hayo ya siku tatu, likinukuu kikosi cha majini cha Jeshi la Ukombozi wa watu wa China.
Akizungumza na shirika la habari la kitaifa la China CCTV, Wang Guangzheng afisa wa Jeshi la Wanamaji amesema doria za pamoja kati ya China na Urusi zimekuza ushirikiano wa kina na wa vitendo kati ya hizo mbili.
China na Urusi zafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi
Luteka hizo zitajumuisha mafunzo ya mazoezi ya silaha za moto za majini, upelelezi na onyo la mapema, utafutaji na uokoaji, na ulinzi wa anga. Hata hivyo haikubainishwa ni wapi kwenye bahari hiyo inayogombaniwa mazoezi hayo yanafanyika.