1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaahidi vitega uchumi zaidi barani Afrika

5 Septemba 2024

Rais wa China Xi Jinping ameahidi msaada wa mabilioni ya dola kwa nchi za Afrika.

https://p.dw.com/p/4kIiQ
Mkutano wa kilele wa China na Afrika
Viongozi wa Afrika zaidi ya 50 pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wanahudhuria mkutano huo wa kilele mjini Beijing.Picha: Andy Wong/AP/picture alliance

Rais wa China Xi Jinping, amefungua mkutano na viongozi wa Afrika mjini Beijing ambapo ameahidi msaada wa mabilioni kwa nchi za Afrika na kusadia kutengeneza nafasi za ajira milioni moja barani Afrika.

Rais Xi amesifu uhusiano wa China na bara la Afrika na ameeleza kuwa uhusiano huo umefikia hatua nzuri kabisa.

China imeahidi kutoa zaidi ya dola bilioni 50 kwa nchi za Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo

Viongozi wa Afrika zaidi ya 50 pamoja na Katibu Mkuu  wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wanahudhuria mkutano huo wa kilele mjini Beijing.

Wakati huo huo China imetiliana saini mikataba kadhaa na Chad na Senegal ya miradi ya umeme, miundombinu na teknolojia ya mawasiliano.