1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yahimiza kuimarishwa kwa juhudi za amani duniani

13 Septemba 2024

Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun, amesema China itaimarisha ushirikiano wa kijeshi na nchi jirani, na kwamba mataifa makubwa yanapaswa kuwa mstari wa mbele kulinda usalama wa kimataifa.

https://p.dw.com/p/4karm
Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun
Waziri wa Ulinzi wa China Dong JunPicha: Florence Lo/REUTERS

Waziri huyo aliyasema hayo katika hotuba yake pana kwenye kongamano la kila mwaka la diplomasia ya kijeshi ya China mjini Beijing.

“Tuko tayari kuendelea kukuza mahusiano mazuri na mataifa makubwa kudumisha maendeleo thabiti ya uhusiano wa kijeshi ili kulinda utulivu wa kimkakati wa kimataifa. Tuko tayari kuendelea kuimarisha uhusiano wa kijeshi na nchi Jirani na kuboresha pande zote kuaminiana. Tuko tayari kulinda usalama wa kikanda, na kutanua uhusiano wa kijeshi na nchi zote.”

Wawakilishi wa  nchi 90 wakiwemo wa mashirika ya kimataifa walihudhuria kongamano hilo la siku tatu linalokamilika kesho Jumamosi.
Ingawa baadhi ya nchi ziliwatuma mawaziri wa Ulinzi kwenye kongamano hilo, mataifa ya Magharibi yalituma maafisa wa ngazi za chini.