1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yahitimisha luteka ya kijeshi karibu na Taiwan

10 Aprili 2023

China leo hii imetangaza kuwa imekamilisha kwa mafanikio siku tatu za mazoezi ya kivita karibu na Taiwan, yaliyojumuisha uoneshaji wa uwezo wa kijeshi na kufanya mazoezi ya kukizingira kisiwa hicho kinachojitawala.

https://p.dw.com/p/4PsbE
USS Milius-Schiff
Picha: U.S. Navy/REUTERS

China leo hii imetangaza kuwa imekamilisha kwa mafanikio siku tatu za mazoezi ya kivita karibu na Taiwan, yaliyojumuisha uoneshaji wa uwezo wa kijeshi na kufanya mazoezi ya kukizingira kisiwa hicho kinachojitawala.

Taarifa ya jeshi la China ilisema wanajeshi wako "tayari kwa vita na wanaweza kupigana wakati wowote, na wataivuruga kwa nguvu aina yoyote ya kile kitachoitwa 'uhuru wa Taiwan' na majaribio ya uingiliwaji wa kigeni".

Marekani, ambayo mara kwa mara imekuwa ikiitaka China ijizuwie kuchukua hatua dhidi ya Taiwan, leo ililipeleka meli ya kivita iitwayo USS Milius kupiga doria katika maeneo yote yanayozozaniwa ya Bahari ya China Kusini.

Mazoezi hayo ya siku tatu yalikuwa jibu la mkutano wa Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen na Spika wa Bunge la Marekani, Kevin McCarthy wa juma lililopita, mkutano ambao ilionya ungesababisha hatua kali za makabiliano.