China yaichokoza India kwa ramani mpya rasmi
30 Agosti 2023Ramani mpya ya kitaifa iliyochapishwa na serikali ya China imezua kilio nchini India, na kuzidisha mvutano kati ya majirani hao wawili wenye silaha za nyuklia.
Toleo la ramani ya Chhina iliyochapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Maliasili inaonyesha wazi jimbo la kaskazini-mashariki la India la Arunachal Pradesh, ambalo Beijing inaliona kuwa sehemu ya Tibet, na Plateau ya Doklam, ambayo pande hizo mbili zimepigania katika miaka ya hivi karibuni, yamejumuishwa ndani ya mipaka ya China, pamoja na Aksai Chin katika sehemu ya magharibi, ambayo China inadhibiti lakini India bado inadai nbi sehemu yake.
Akijibu madai ya China, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya India alisema: "Tunakataa madai haya kwa kuwa hayana msingi."
Waziri wa Mambo ya Nje Jaishankar Subhramanyam pia alitupilia mbali ramani hiyo mpya, akisema, "kutoa madai ya kipuuzi kwenye eneo la India hakufanyi kuwa eneo la China."
Mwanasiasa wa upinzani nchini India Rahul Gandhi alimtaka Waziri Mkuu Narendra Modi kujibu madai ya China.
Ramani kama silaha za kisiasa
Kuchapisha kwa China kwa ramani hiyo mpya, na malalamiko kuliyosababisha nchini India, ni mfano wa jinsi ramani zinavyoweza kutumika kuonyesha nguvu.
Soma pia: Wang Yi afanya ziara rasmi India
Tim Trainor ni mwenyekiti wa Chama cha Kimataifa cha Katografia na mwanachama mwanzilishi wa Kamati ya Wataalamu ya Umoja wa Mataifa juu ya Usimamizi wa Taarifa za Ulimwengu wa Geospatial. Aliiambia DW kuwa ramani zinaweza kuathiri jinsi watu wanavyofikiri kuhusu sehemu za dunia.
"Ramani zina nguvu sana na unajua watu wengi wanapotazama ramani, wasomaji wengi wa ramani hudhani kuwa taarifa wanazozitazama ni sahihi," alisema.
Sawa na nambari na takwimu ambazo zinaonekana kuwa na lengo, lakini hazihitajiki kuwa sahihi, ramani zinatumika hasa kama zana za propaganda.
Mwandishi wa Ujerumani Ute Schneider anaandika katika kitabu chake "The power of maps" kwamba hakuna ramani zisizoegemea upande au "zisizopendelea" kwa sababu "ramani ni zana za kuoyesha nguvu."
Hii inatumika pia kwa ramani zinazotolewa na serikali ya India. Zinaonyesha, kama jambo la hakika, "kichwa" cha India - ikimaanisha eneo la Kashmir, ambalo India na Pakistani, na kwa kiasi kidogo Uchina, zinagombania.
Siasa za kisasa za jiografia zinazoathiri eneo hili zilianzia himaya ya Uingereza nchini India, na "jimbo la kifalme" la Jammu na Kashmir ambalo lilivunjwa kufuatia kugawanywa kwa India mnamo 1947.
Soma pia: Mzozo Kashmir: Waziri wa Mambo ya Nje wa India azuru China
Hata hivyi ramani haionyeshi migogoro ya eneo, na ukweli kwamba sehemu kubwa ya Kashmir inayodaiwa kuwa ya "India" inasimamiwa na Pakistan na China. Kinyume chake, ndivyo ilivyo pia kwa Pakistan.
Wahindi wengi hujifunza kuhusu mzozo huu wa kijiografia na kisiasa kwa mara ya kwanza wakiwa watu wazima baada ya kuusoma katika machapisho ya kigeni au kuona ramani zinazotolewa nje ya nchi. Nchini India, kusambaza ramani ambazo hazionyeshi toleo "rasmi" la jiografia kunaweza kusababisha mashtaka ya jinai.
Nchini Pakistan, suala la Kashmir linagusa vile vile. Kwenye ramani rasmi, Jammu na Kashmir imejumuishwa kama eneo la Pakistan. Hata hivyo, kinyume na ramani za India, ramani za Pakistani zinaonyesha hali ya kutatanisha ya maeneo ya mpaka kwa maneno kama "eneo lenye migogoro" na "mpaka usiobainishwa" yaliyochapishwa kwenye ramani.
Uchoraji wa utaifa
India, China na Pakistan sio nchi pekee zinazotumia ramani kama zana za propaganda. Nchi nyingi za Asia huchapisha ramani rasmi zenye jiografia ambazo zina uhusiano wa muda mfupi na usahihi.
Katika muktadha huu, haishangazi kuona ramani kuwa suala la ubishani kati ya nchi.
Katika mzozo kuhusu Bahari ya China Kusini, kwa mfano, kunakuwa na mizozo kuhusu ramani zinazoonyeshwa kwenye filamu. Hivi karibuni, sinema ya Hollywood "Barbie" ilipigwa marufuku nchini Vietnam kwa sababu inadaiwa ilionyesha kile ambacho Hanoi alikichukulia kama ramani isiyo halali ya Bahari ya Kusini ya China.
Mnamo mwaka wa 2019, nchi kadhaa za Kusini-mashariki mwa Asia zilikosoa vikali filamu ya "Abonable" kwa tukio ambalo ramani inayoonyesha tafsiri tata ya China kuhusu Bahari ya China Kusini ilionekana nyuma.
Ramani ilionyesha "mstari wa dashi tisa," ambao unaonyesha Taiwan yote na Bahari ya China Kusini kama eneo la China.
China inadai mamlaka ya kihistoria, lakini Taiwan na nchi jirani zinakataa madai ya Beijing ya kumiliki ardhi katika eneo hilo. Mnamo mwaka wa 2016, mahakama ya kimataifa iliamua kwamba madai ya china katika Bahari ya China Kusini sio halali chini ya sheria za kimataifa za baharini.
Chanzo: DW