1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

China yaitaka Marekani kuacha kukandamiza maendeleo yake

23 Desemba 2022

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, ameitaka Marekani kuacha kukandamiza maendeleo ya China na haipaswi kuendeleza utaratibu wake wa zamani wa uonevu wa upande mmoja.

https://p.dw.com/p/4LMsD
US EU Handel TTC Washington
Picha: Saul Loeb/AP/picture alliance

Wang Yi ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken.

Amebainisha kuwa Marekani lazima izingatie masuala halali ya China.

Wang amesisitiza kwamba nchi hizo mbili zinapaswa kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi zilizoendelea na zinazoinukia kiuchumi, G20 mjini Bali, baina ya Rais wa China, Xi Jinping, na mwenzake wa Marekani, Joe Biden.

Wang amesema ni muhimu kuongeza mashauriano juu ya mwongozo wa kanuni za uhusiano kati ya China na Marekani, kuimarisha mazungumzo katika nyanja zote na kutatua masuala muhimu kati ya nchi hizi mbili.