1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yapinga Marekani kuziwekea vikwazo kampuni zake

15 Februari 2023

China imesema itachukua hatua za kulipiza kisasi dhidi ya kampuni za Marekani zitakazohujumu uhuru wa China.

https://p.dw.com/p/4NUul
China I Wang Wenbin I Sprecher des chinesischen Außenministeriums
Picha: Kyodo/picture alliance

Msemaji wa Wizara ya mambo ya kigeni ya China Wang Wenbin amesema hayo, baada ya Marekani kulidungua puto la China na kutangaza kuwa itaziwekea vikwazo kampuni sita zinazohusishwa na mpango unaoshukiwa wa ujasusi wa China.

China yaiahidi Iran uungwaji mkono thabiti

Wenbin amewaambia waandishi habari kuwa Marekani imetumia vibaya nguvu, na kuhamaki kupita kiasi, na kutumia tukio hilo kama kisingizio cha kuziwekea vikwazo kinyume cha sheria kampuni na taasisi za China.

Ameongeza kuwa China italinda uhuru wake na haki zake halali pamoja na maslahi.