1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yatanua luteka za kijeshi karibu na Taiwan

11 Desemba 2024

China imetanua luteka zake za kijeshi karibu na kisiwa cha Taiwan, ikilenga kuweka kile kinachoonekana kama mstari mwekundu, kwa rais mpya ajaye nchini Marekani.

https://p.dw.com/p/4nzVX
Taiwan | Ndege ya kivita ya Taiwan kikipaa
China yafanya luteka za kijeshi karibu na visiwa vya kusini mwa Japan zikihusisha takriban meli 60 za kivita na meli 30 za walinzi wa pwani.Picha: Chiang Ying-ying/AP/picture alliance

Hayo yameripotiwa na mamlaka za Taiwan Jumatano, zikisema serikali ya Beijing inataka kuleta matatizo.

Afisa mmoja mwandamazi katika masuala ya usalama wa taifa,ambaye hakutaka kutajwa  jina, ameliambia shirika la habari la AFP, kwamba Luteka kubwa za kijeshi zinazofanywa na Beijing ambazo hazijawahi kuonekana kwa kipindi cha miaka kadhaa zinahusisha kiasi meli 60 za kivita na meli 30 za walinzi wa pwani.

Luteka hizo zinafanyika karibu na visiwa vya Kusini mwa Japan hadi bahari ya Kusini mwa China.

Kadhalika China imeimarisha shughuli za kutumia ndege za kijeshi karibu na kisiwa cha Taiwan katika kipindi cha siku mbili zilizopita.