1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Croatia kuanza kutumia sarafu ya euro kuanzia Januari 2023

13 Julai 2022

Croatia itaanza kutumia sarafu ya euro kuanzia Januari 2023 baada ya kukamilisha leo hatua za mwisho kabisa za kisheria mjini Brussels ili kukubaliwa kutumia sarafu hiyo ya pamoja ya Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4E53C
Brasilien USA EU Dollar Euro als Zahlungmittel
Picha: AP

Waziri wa Fedha wa Croatia Zdravko Maric amesema ana furaha kuiona nchi yake ikihamia katika matumizi ya sarafu ya euro licha ya changamoto kubwa kabisa za mfumko wa bei na ukuaji mdogo wa uchumi nchini mwake.

Mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya wamekutana leo mjini Brussels kutoa idhini ya mwisho kwa vipengele vitatu vya kisheria ili kuikubalia Croatia kuwa mwanachama wa kanda ya euro, ambayo ni kundi la nchi za Umoja wa Ulaya zinazotumia sarafu hiyo ya pamoja.

Christine Lagarde ni rais wa Benki Kuu ya Ulaya. Kuingia kwa Croatia kunaandamana na uungwaji mkono wa Halmashauri Kuu ya Ulaya na Benki Kuu ya Ulaya baada ya nchi hiyo kutimiza vigezo muhimu vya muunganiko.