DAVOS : Abbas akutana na Livni
26 Januari 2007Waziri wa mambo ya nje wa Isarel Zipi Livni na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina wamekuwa na mazungumzo pembezoni mwa Kongamano la Kiuchumi Duniani mjini Davos Swirtzerland.
Livni amesema katika hotuba hapo jana kwamba amani ya kudumu ni matumaini ya watu wake na kuahidi kwamba taifa la Wapalestina la kipindi cha usoni ni jambo linaloweza kufanikishwa Amemtaka Abbas kutowaridhia watu wenye siasa kali akimaanisha wanamgambo wa serikali ya Hamas wanaorudia kutowa wito wa kuangamizwa kwa taifa hilo la Kiyaudi.Amesema serikali yake haitokubali kujadili haja ya usalama kwa nchi yake.
Abbas amesema ana imani kwamba mchakato wa amani utarudishwa kwenye mkondo wake. Abbas na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert wanatazamiwa kuwa na mazungumzo mwezi ujao na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice.