DAVOS: Mataifa yakubaliana kuanza tena mashauriano ya biashara huru duniani.
28 Januari 2007Matangazo
Mataifa makubwa yamekubaliana kuanza tena mashauriano ya biashara huru duniani yaliyosimamishwa miezi sita iliyopita.
Mashauriano hayo yalisimamishwa baada ya makabiliano kati ya mataifa maskini yakiongozwa na Brazil kwa upande mmoja, na Umoja wa Ulaya na Marekani kwa upande mwengine, kuhusiana na mazao ya shambani.
Mawaziri wa biashara wa mataifa thelathini waliokutana mjini Davos, wameelezea matumaini yao kwamba mazungumzo hayo yatafanikiwa.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, amesema wakati huu kuna haja kubwa zaidi kwa mataifa hayo kuafikiana.
Wapatanishi wanatarajiwa kukutana kesho kwenye makao makuu ya Shirika la Biashara la Dunia, WTO, mjini Geneva kuzungumzia kuanzishwa tena duru ya mazungumzo ya Doha.