DAVOS: Mazungugmzo ya WTO yafufuliwe kwa haraka
27 Januari 2007Matangazo
Mawaziri kutoka nchi 24 zenye usemi mkubwa katika sekta ya biashara ambao wanahudhuria Kongamano la Kiuchumi Duniani mjini Davos,Uswissi,wameunga mkono kufufua kwa haraka mazungumzo ya utandawazi yaliokwama.Azma ya mkutano uliofanywa pembezoni mwa Kongamano hilo,ni kutafuta njia ya kuendelea upya na majadiliano ya miaka mitano ambayo yalivunjika mwezi wa Julai mwaka 2006.Mkuu wa WTO -Shirika la Biashara Duniani,Pascal Lamy aliahirisha mazungumzo hayo kwa sababu,mara kwa mara,maoni tofauti kati ya Umoja wa Ulaya, Marekani na nchi zinazoendelea kuhusu ushuru wa forodha,yalikwamisha majadiliano.Kamishna wa biashara wa Umoja wa Ulaya,Peter Mandelson ametoa mwito kwa pande zote zilizohusika kujitolea zaidi katika miezi ijayo.