1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAVOS:Kansela Merkel kufungua rasmi mkutano wa WEF

24 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYJ

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anajiandaa kufungua rasmi Kongamano la masuala ya Uchumi linalofanyika mjini Davos,Uswisi leo baadaye.Bi Merkel anatarajiwa kutoa hotuba inayoelezea mipango yake wakati nchi yake ya Ujerumani inapoanza majukumu yake kama mwenyekiti wa kundi la mataifa nane yaliyostawi kiviwanda G8.Ajenda yake inatilia maanani haja ya kudhibiti athari za mabadiliko ya hali ya anga vilevile kufufua mazungumzo ya biashara ya ulimwengu.Viongozi wa kibiashara vilevile wa kisiasa wameanza kuwasili mjini Davos kunakofanyika mkutano huo.Zaidi ya wajumbe 200 kutoka mataifa 90 wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho huku makampuni yanayochangia takriban robo ya pato lote la ulimwengu kuwakilishwa.