Deutsche Bank yapata viongozi wapya
31 Mei 2012Kuanzia hapo kesho benki hiyo kubwa kabisa nchini Ujerumani itaongozwa na watu wawili Anshu Jain na Jürgen Fitschen.
.Wenye hisa zaidi ya alfu tano katika Benki hiyo ya Ujerumani wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa mwaka wa Benki hiyo ambapo wenyeviti wenza watakaoiongoza watatambulishwa mjini Frankfurt. Pamoja na Mjerumani Jürgen Fitschen ni Anshu Jain kutoka India.
Siyo lazima kiongozi wa benki hiyo awe Mjerumani na hivyo moja kwa moja kuweza kuwa mshirika muhimu wa mazungumzo na serikali ya Ujerumani. Dhima hiyo ilitimizwa na viongozi waliotangulia Hermann-Josef Abs,Alfred Herrhausen na Josef Ackermann ambaye ni Mswisi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel hata alifikia hatua ya kuandaa tafrija kwa heshima ya bwana Ackermann aliekuwa anatimiza umri wa miaka 60 japo hafla hiyo haikupita bila ya utata.
Lakini Bwana Ackermann anaagwa baada ya kuiongoza Deutsche Bank kwa muda wa miaka kumi. Jee wanaomfuatia wanazo sifa kama zake?
Christoph Schalast kutoka chuo cha usimamizi wa fedha cha mjini Frankurt amesema kuwa kwanza inapasa mtu afanye kazi ili kuzifikia sifa hizo, inapasa kufanya afanye kazi ili kujenga imani na mtu mkimya kwa kiasi cha kutosha.Bwana Schalast ameeleza kuwa haipasi kwa mtu kuwa mbinafsi mwenye tabia ya kujinufaisha yeye mwenyewe, anatakiwa awe na uwazi na awe mshauri wa dhati . Amesema watakaomfuatia watakuwa na changamoto ya kuonyesha kwamba wanayaweza hayo.
Watakaomfuatia, Jürgen Fitschen na Anshu Jain watakuwa na jukumu la kuwasaidia wenye hisa katika kupata faida ya hisa zao. Wakati wa uongozi wa Ackermann thamani ya hisa zilipanda na kushuka. Mwanzoni kabisa wakati Ackermann alipokuwa msemaji wa bodi ya uongozi hisa zilikuwa na thamani ya Euro 76.
Mnamo mwaka wa 2007 zilivuka thamani ya Euro 118 lakini hadi kufikia mwezi januari mwaka 2009 thamani ilishuka hadi Euro 15 tu. Kwa jumla, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita thamani ya hisa za Deutsche Bank imeanguka kwa asilimia 60.Kwa hiyo ilikuwa vizuri kwa wateja walioziweka fedha zao katika vitabu vya akiba ya benki kwa njia ya kawaida.
Ili kuibadilisha hali hiyo itapasa katika siku za neema kuwekeza katika shuhguli za kuzalisha mitaji. Lakini katika hilo Deutsche Bank ilikabiliwa na tajiriba mbaya wakati wa mgogoro wa mabenki ulioikumba dunia.. Badala ya kuwa mdhamini wa mashaka ikawa mfanya biashara za mashaka na ilipeleka dhamana nyingi za mashaka kwenye soko.
Viongozi wapya watakuwa na changamoto ya kutafuta wizani baina ya ugeugeu katika vitega uchumi katika uzalishaji wa mitaji na biashara imara na makampuni na wateja binafsi. Chini ya uongozi wa Ackermann kulikuwa na mpango wa kuzalisha nusu ya mapato kutokana na kuwekeza katika shughuli za kuzalisha mitaji -investment banking.
Mwandishi:Braun,Michael
Tafsiri;Mtullya Abdu
Mhariri:Hamidou Oummilkheir