1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dhoruba Ciaran yaua watu 7 magharibi mwa Ulaya

3 Novemba 2023

Watu wasiopungua 10 wamekufa na wengine wamejeruhiwa, baada ya dhoruba "Ciaran" kupiga Ulaya Magharibi.

https://p.dw.com/p/4YM3x
Mawimbi ya baharini yaruka futi kadhaa juu baada ya kupiga ukuta wa jengo ufuoni mwa bahari kule Newhaven, kusini mwa England Novemba 2, 2023, wakati kimbunga Ciaran kilipopiga Uingereza.
Mawimbi ya baharini yaruka futi kadhaa juu baada ya kupiga ukuta wa jengo ufuoni mwa bahari kule Newhaven, kusini mwa England Novemba 2, 2023, wakati kimbunga Ciaran kilipopiga Uingereza.Picha: Glyn Kirk/AFP

Uholanzi, Ubelgiji, Ujerumani, Ufaransa na Italia zilishuhudia upepo mkali, mafuriko, kukatika kwa umeme huku huduma za usafiri zikisitishwa kwa muda.

Kimbunga hicho kilichopiga kwa kasi ya hadi  kilometa 200 kwa saa kilipelekea takriban kaya milioni 1.2 kukosa umeme huku mamia kwa maelfu ya watu wakikosa mawasiliano ya simu zao za mkononi.

Mamia ya safari za ndege na treni ziliahirishwa kutokana na dhoruba hiyo.

Dhoruba Ciaran ilipiga pia kusini mwa Uingereza ambako mamia ya shule zilifungwa.

Katika kisiwa cha Jersey, baadhi ya wakazi walilazimika kuhamishwa hadi hotelini kutokana na mafuriko.