1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dhoruba ya theluji yaikumba Marekani

9 Februari 2013

Dhoruba kali ya theluji imeshambulia kaskazini-mashariki mwa Marekani siku ya Ijumaa, na kuvuruga usafiri na kupelekea magava watano wa majimbo kutangaza hali ya dharura.

https://p.dw.com/p/17bH4
Kimbunga cha Sandy.
Kimbunga cha Sandy.Picha: STAN HONDA/AFP/Getty Images

Mji wa Boston ulitabiriwa kufunikwa na theluji kubwa.Watabiri wa hali ya hewa wamesema maeneo mengi ya mji huo yanaweza kushuhudia theluji yenye ukubwa wa futi mbili (sentimita 60), na mengine yakishuhudia ukubwa wa inchi 30 (sentimita 76). Mji wa New York ulitarajiwa kupata karibu sentimita 30 katika baadhi ya maeneo, wakati theluji kubwa ilitarajiwa kuanguka katika miji ya majimbo ya Connecticut na Maine.

Ndege ya shirika la ndege la Marekani inavyoonekana wakati kimbunga cha theluji kikishambulia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Philadelphia.
Ndege ya shirika la ndege la Marekani inavyoonekana wakati kimbunga cha theluji kikishambulia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Philadelphia.Picha: AP

Upepo ulikuwa unapuliza kwa kasi ya kilomita 56 hadi 64 kwa saa kufikia mchana wa Ijumaa na watabiri walitarajia kasi hiyo kuongezeka na kufukia kilomita 97 kwa saa wakati kufikia jioni. Hali ya uendeshaji ilijuwa ya hatari. Gavana wa jimbo la Massachusetts Daval Patrick alichukua hatua isiyo ya kawaida kwa kutangaza marufuku kwa usafiri mwingi wa magari kuanzia mchana wa Ijumaa, wakati gavana wa Connecticut Dannel Malloy alifunga barabara kuu za jimbo kwa matumizi ya magari isipokuwa maghari ya dharura tu.

Hadi kufikia jioni, huku theluji ikizidi, usafiri wa magari yanayopita pia uliathiriwa. Mjini New York maafisa wanaoshughulikia usafiri wa kupita walisema uwezekano wa kusitisha huduma ni mkubwa, na Reli ya Metro-North ilisimamisha baadhi ya huduma zake za abiria saa nne usiku. Reli ya Long Island pia ilisimamisha baadhi ya huduma katika tawi lake la Montauk.

Huduma ya umeme yakatika

Dhiruba hiyo iliacha karibu wateja 10,000 katikapwani ya mashariki bila umeme, safari karibu 3,500 na ndege zilifutwa. "Tunashuhudia theluji kubwa ikifunika kanda kuanzia kusini hadi kaskazini," alisema Lance Franck, Afisa anayehusika na upimaji wa hali ya hewa katika kituo cha taifa cha hali ya hewa mjini Taunton, Massachusetts, nje ya Boston.

Mapema Ijumaa jioni, maafisa walionya kuwa kimbunga hicho ndiyo kwanza kilkuwa kinakusanya nguvu zake kamili, na kwamba theluji kubwa na upepo mkali unaweza kuendelea hadi mchana wa Jumamosi. Magavana wa Massachusetts, Rhode Island, Conncecticut, New York na Maine walitangaza hali za dharura na kuwataka raia kubakia ndani ya majumba yao.

Miti iliyoko mataa wa Pennsylvania, kuelekea jengo la bunge la Capitol Hill, ikiwa imefunikwa na theluji.
Miti iliyoko mataa wa Pennsylvania, kuelekea jengo la bunge la Capitol Hill, ikiwa imefunikwa na theluji.Picha: AP

katika hali nyingi mamlaka ziliwaagiza wafanyakazi wa serikali wasiyo muhimu sana kubakia nyumbani, na kuwashauri waajiri binafsi kuchukua hatua sawa, pia watu walitakiwa kujiandaa kwa kukatika umeme, na kuwahamasisha kuwajulia hali majrani zao wazee na wasiyojiweza. Watu walionekana kuchukulia onyo hizo kwa umakini. Magari katika mitaa na wasafiri katika usafiri wa umma walikuwa wachache kuliko kawaida siku ya Ijumaa.

"Hiki ni kimbunga kikubwa na chenye nguvu, lakini tunatiwa moyo na idadi ya watu waliobakia nyumbani leo," alisema Meya wa Boston Thomas Menino wakati akizungumza na waandishi wa habari. Mjini New York, Meya Michael Bloomberg alisema kimbunga hicho kilitoa nafasikwa watu kupumzika na kulala. Pamoja na hayo, kimbunga hicho kilisababisha ajali ndogo ukiwemo msongamano wa magari 19 nje ya mji wa Portland, Maine, ambao ulipelekea mtu mmoja kufikishwa hospitali.

Kwa wengine theluji ni habari njema

Kimbunga hicho hakikuwa habari mbaya kwa kila mmoja. Alipopata habari kuhusu theluji yenye upana wa inchi 8 hadi 10 katika mlima wa Elk mjini Uniondale, Pennsylvania, mchezaji wa mchezo wa kuteleza kwenye theluji Sophia Chesner mwenye umri wa miaka 8 kutoka Mooretown, New Jerssay, ambaye alikuwa katika likizo ya mchezo huo pamoja na familia yake alifurahia. Mdogo wake Giuliana mwenye umri wa miaka 4 alisema haijalishi uzuri wa mchezo wa kuteleza, yeye alikuwa na vipaumbele vingine mara tu theluji hiyo itakapojaa. "Jambo la kwanza nakwenda kujenga sanamu la theluji (Snowman) na kutafuta nyayo za Sasquatch," alisema Guiliana Chesner.

Hali ilivyo katika uwanja wa Time Square.
Hali ilivyo katika uwanja wa Time Square.Picha: picture-alliance / dpa

Lakini maisha hayakuwa rahisi kwa wale waliokuwa wamepanga kusafiri.Pamoja na kufutwa kwa safari za ndege siku ya Ijumaa, safari nyingine zaidi ya 1,200 zilizopangwa siku ya Jumamosi zilifutwa kwa mujibu wa tovuti ya FlightAware.com. Kimbunga hicho pia kimesababisha hofu ya mafuriko kwa maeneo yaliyoathriwa na kimbunga cha Sandy Oktoba mwaka jana. Bloomerg alisema baadhi ya watu walioathiriwa na kimbunga hicho karibu siku 100 zilizopita, wanaweza kushuhudia mafuriko ya wastani katika pwani. Mji wa Brick katikajimbo la New Jersey ulikuwa na wafanyakazi wakirundika mchanga na vizuizi kujiandaa na ongezeko la ukali wa kimbunga hicho.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef