Die Linke chatangaza wagombe uchaguzi wa mapema Ujerumani
10 Novemba 2024Matangazo
Mwenyekiti mwenza wa chama hicho Jan van Aken na mbunge Heidi Reichinnek ndiyo watakiongoza kwenye kiny'anganyiro hicho.
Soma zaidi:Uchaguzi wa Ujerumani unafanyikaje?
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari kiongozi mwenza Ines Schwerdtne amesema wanaingia kwenye kampeni za uchaguzi wakiwa kitu kimoja akiashiria kuwa wagombea wamepitishwa kwa sauti moja.
Chama hicho cha mrengo wa kushoto, kimeporomoka katika uungwaji mkono tangu mmoja wa viongozi wake wa ngazi ya juu Sahra Wagenknecht alipojiondoa na kuanzisha chama chake kilichobeba jina lake. Kwa sasa bado haifahamiki ikiwa Die Linke kitavuka kihunzi cha kupata asilimia 5 inayohitajika kuingia bungeni.