1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Mahakama ya New York yasema Trump alidanganya benki na bima

27 Septemba 2023

Mahakama ya New York imetoa uamuzi jana Jumanne kwamba aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump alifanya ulaghai katika shughuli zake za biashara katika muongo mmoja uliopita.

https://p.dw.com/p/4WqML
Donald Trump baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara wa kusaka fedha za ufadhili wa kongamano la GOP, Alabama.
Donald Trump baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara wa kusaka fedha za ufadhili wa kongamano la GOP, Alabama.Picha: Butch Dill/AP/picture alliance

Jaji Arthur Engoron, alipokuwa akitoa uamuzi wa kesi hiyo iliyowasilishwa na mwanasheria mkuu wa serikali wa New York Letitia James, amesema Trump na kampuni yake waliidanganya benki, makampuni ya bima na wengineo kwa kutoa tathmini ya uongo ya mali zake ili kupata mikataba na mikopo.

Jaji Engoron aidha ameamuru kufutwa baadhi ya leseni za biashara za Trump kama adhabu na kumuwekea mazingira magumu ya kufanya biashara mjini New York.

Wakili wa Donald Trump Christopher Kise amesema wanaweza kuukatia rufaa uamuzi huo aliouita "upotoshaji wa haki" na usiozingatia ukweli na sheria.

Trump kwa muda mrefu amekuwa akisisitiza hajafanya kosa lolote.