1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Donald Tusk atarajiwa kuwa waziri mkuu wa Poland

11 Desemba 2023

Wabunge nchini Poland wamekusanyika katika kikao maalum cha bunge ambapo rais wa zamani wa baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk anatarajiwa kupewa jukumu la kuunda serikali mpya nchini humo.

https://p.dw.com/p/4a21l
Ukumbi wa Bunge la Poland mjini Warsaw
Kiongozi wa upinzani nchini Poland, Donald Tusk (katikati) anajiandaa kuchukua uongozi wa nchi hiyo.Picha: Michal Dyjuk/AP/picture alliance

Spika wa bunge Szymon Holownia kutoka chama cha kiliberali cha Third Way amesema, leo itakuwa siku muhimu katika historia ya Poland.

Kwa kipindi cha miaka minane nchi hiyo imekuwa chini ya utawala wa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia.

Hata hivyo rais anayeondoka madarakani Andrezej Duda ambaye ni mshirika wa serikali inayoondoka  kwanza amekikabidhi chama cha sheria na Haki jukumu la kuunda serikali, kikiongozwa na waziri mkuu Mateusz Morawiecki.

Ikiwa serikali hiyo haitopata uungwaji mkono wa kutosha wabunge watamteua mgombea mwingine kuchukua nafasi ya waziri mkuu na inaelezwa kwamba wameshajiandaa kumpa nafasi hiyo Donald Tusk.