DRC yadai askrai 500 wa Rwanda wameingia nchini mwake
9 Juni 2022Katika taarifa yake ya jana jioni, jenerali Sylvain Ekenge ambaye ni msemaji wa gavana wakijeshi hapa Kivu ya Kaskazini amefahamisha hayo wakati alipokua akiwafahamisha waandishi wa habari kuhusu wanajeshi wa Rwanda walioingia upya nchini Kongo na walioonekana kwenye milima ya Chanzu wilayani Rutshuru wakiwa wamevalia sare aina mpya tofauti na kama inavyokuwa kawaida kwa askari wa nchi hiyo jirani na Congo.
Rwanda yasema iko tayari kulipiza kisasi iwapo Congo itashambulia tena
Kulingana na ushuhuda wa wakazi wa maeneo hayo hayo, mamia ya askari wa jeshi la Rwanda walionekana kwenye mizunguko ya mlima mrefu wa Chanzu ambao umekua ni ngome muhimu ya kundi la waasi wa M23.
Hata hivyo, upande wa viongozi wa mashirika ya kiraia ambayo pia yamethibitisha kuweko kwa askari hao akiwemo Jean Claude Bambanze ambaye ni mkuu wa mashirika ya kiraia wilayani Rutshuru, wamezitaka serikali zote hizo mbili zinazo laumiana kuingia kwenye mazungumzo ili kuondoa tofauti zinazoshuhudiwa hivi sasa.
Kongo yaishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23
Hali imekuwa ni ya wasiwasi katika baadhi ya maeneo wilayani Rutshuru na nyiragongo ambamo mzozo huo katika ya nchi hizi mbili umesababisha maelfu ya raia kuvitoroka vijiji vyao ili kupata hifadhi katika makambi nje kidogo na mji wa Goma.
Kwa muda mrefu serikali ya kigali imekuwa ikiilaumu kinshasa kwakuwahifadhi waasi wa FDLR ambao ni tishio kubwa kwa nchi hiyo . katika mazungumzo yake pamoja na raisi wa angola mapema mwanzoni mwa juma hili, Rais Tshisekedi alithibitisha kuhusu Rwanda kulisaidia kundi la waasi wa M23 hali inayo endelea kuongeza utata kati ya mataifa haya mawili .