1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRESDEN:Kansela Schröder na Merkel waelekea jimbo la Dresden

30 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEWH

Viongozi wa vyama viwili vikuu vya kisiasa wanaelekea eneo la Mashariki ya Ujerumani la Dresden ambako uchaguzi unatarajiwa kufanyika jumapili ijayo.

Uchaguzi kwenye eneo hilo ulihairishwa kwa majuma mawili baada ya kifo cha mgombea wa chama cha NDP.

Wataalamu wanasema matokeo ya uchaguzi kwenye eneo hilo hayaonyeshi uwezekano wa kubadili mizani ya uongozi kati ya Chama cha Kansela Gerhard Schröder cha Social Demokrats na Christian Demokrats cha Angela Merkel ambacho kwa sasa kinawingi wa viti vitatu bungeni.

Vigogo wote wawili Schroder na Merkel wanatazamiwa kuhutubia mikutano baadae hii leo.

Mapema kiongozi wa Social Demokrats Franz Münterfering alikanusha kwamba Schröder amepanga kukataa kuwania kiti cha Ukansella jumatatu wakati wa kusherehekea siku ya muungano wa Ujerumani.