1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Droo ya ligi ya mabingwa yapangwa

18 Desemba 2023

Droo ya 16 bora ya ligi ya mabingwa imeshuhudia timu nane zilizomaliza katika nafasi ya juu kwenye makundi zikipangwa dhidi ya mmoja wa washindi nane waliomaliza nafasi ya pili.

https://p.dw.com/p/4aIu4
Champions League - Round of 16 Draw
Picha: UEFA/Handout via REUTERS

Timu tatu kati ya nne za Bundesliga zimefuzu katika hatua ya mtoano ya Ligi ya mabingwa Ulaya,  huku Bayern Munich, Borussia Dortmund na RB Leipzig zikitinga hatua ya 16 bora. Union Berlin pekee ndiyo iliyoshindwa kufuzu katika kundi lao.

Kutoka hapa Ujerumani RB Leipzig itachuana  na Real Madrid,Bayern Munich itacheza na Lazio na  mwakilishi mwengine kutoka ujerumani Borussia Dortmund acheze na PSV Eindhoven ya Uholanzi.

Mabingwa watetezi Manchester City wamepangwa kukutana na Copenhagen, wanaofikia katika hatua hii kwa mara ya kwanza tangu 2011.

UEFA Champions League | Finale | Manchester City vs Inter Mailand
Manchester City mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwaPicha: Manu Fernandez/AP Photo/picture alliance

Soma pia: Droo ya hatua ya 16 yafanywa

Porto itakutana na Arsenal. Paris Saint-Germain imepata afueni baada ya kuorodheshwa katika kundi la "kifo" ambapo ilimaliza katika nafasi ya pili itakabiliana na Real Sociedad itakayocheza katika msimu wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa katika muongo mmoja.

Mabingwa wa ligi ya Italia Napoli watashuka dimbani na Barcelona. Mechi za mkondo wa kwanza zimeratibiwa kuchezwa Februari 13 mwaka 2024, kisha za marudiano mnamo Machi 5.

Droo ya ligi ya Ulaya

FC Villarreal - Manchester United | Europa League | Finale
Kombe la ligi ya UlayaPicha: Rafal Oleksiewicz/dpa/PA Wire/picture alliance

Katika droo ya ligi ya Ulaya hatua ya mchujo,  AS Roma itakutana kwa mara nyengine tena na Feyenoord. Roma iliishinda Feyenoord katika fainali ya Europa Conference msimu wa mwaka  2021-22, na timu hizo pia zilikutana kwenye Ligi ya Ulaya msimu uliopita katika hatua ya robo fainali, huku Roma wakiibuka kidedea, kwa jumla ya mabao 4-2.

Roma, inayonolewa na kocha Jose Mourinho, ilitinga fainali ya mashindano hayo msimu uliopita lakini ilipoteza dhidi ya Sevilla kupitia mikwaju ya penalti. 

Ungarn, Budapest | Sevilla gewinnt das Europa League Finale gegen Roma
Sevilla wakishangilia ushindi wa ligi ya Ulaya msimu wa 2022/23.Picha: Petr David Josek/AP Photo/picture alliance

Soma pia: Droo ya hatua ya makundi Champions League

AC Milan itacheza na Stade Rennes, RC Lens iakipiga na Freiburg, Young Boys itakutana na Sporting Lisbon huku  Benfica ikitarajia kuchuna na Toulouse

Sporting Braga itacheza na Qarabag, nayo Galatasaray ikipige na Sparta Prague, Shakhtar Donetsk itakutana na Olympique de Marseille.

Timu zilizomaliza katika nafasi ya pili kwenye hatua ya makundi ya Europa League, zinacheza mechi za mtoano na timu zilizomaliza kwenye nafasi ya tatu katika hatua ya makundi ya Champions League na atakayeshinda anafuzu raundi ya mtoano ya 16 ambapo atapangiwa kucheza na timu zilizoshinda makundi kwenye hiyo Europa League.

Kwa sasa West Ham United, Brighton , Rangers, Atalanta, Liverpool, Villareal, Slavia Prague na Bayer Leverkusen wamefuzu kwa hatua ya 16 bora ya europa League kwa kuwa walikuwa washindi wa makundi yao.

Mechi za kwanza zitachezwa Februari 15, na mechi za marudiano wiki moja baadaye mnamo Februari 22.