1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru ya pili ya uchaguzi wa urais Uturuki kufanyika Mei 28

15 Mei 2023

Wapinzani wa Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kumaliza utawala wake wa miongo miwili madarakani katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais mnamo Mei 28.

https://p.dw.com/p/4RMHO
Türkei Wahlen | Parteizentrale AKP
Picha: Ali Unal/AP Photo/picture alliance

Hii ni baada ya Erdogan kupata matokeo mazuri kuliko ilivyotarajiwa katika duru ya kwanza ya upigaji kura jana Jumapili japo ameshindwa kupata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa.

Uungwaji mkono kwa Erdogan ulikuwa chini kidogo ya asilimia 50 inayohitajika kisheria ili kuizuia nchi hiyo mwanachama wa NATO kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi ambao unachukuliwa kama mtihani kwa utawala wake.

Rais wa Uturuki atambua uwezekano wa kufanyika duru ya pili ya uchaguzi nchini mwake.

Vyombo vya habari vinavyoiunga mkono serikali vimeonekana kufurahia matokeo hayo huku gazeti la Yeni Safak likiandika kichwa cha habari "Watu Wameshinda," kuashiria muungano wa Erdogan wa People's Alliance ambao unaonekana kushinda viti vingi bungeni.