SiasaNigeria
ECOWAS yaombwa kutathmini hatua zake za kushughulikia mizozo
24 Februari 2024Matangazo
Tinubu amesema jumuiya hiyo inapaswa kuzingatia mabadiliko hayo ili kuweza kuyarejesha mataifa yaliyojitoa kwenye muungano huo.
Amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo unaofanyika mjini Abuja.
Viongozi hao wanakutana kuzungumzia mzozo wa kisiasa katika ukanda huo uliokumbwa na mapinduzi ya kijeshi na kuchochewa na hatua ya mwezi Januari ya Niger, Burkina Faso na Mali kujitoa kwenye jumuiya hiyo yenye wanachama 15.
Ingawa hakufafanua zaidi, lakini matamshi ya Tinubu huenda yakaongezea nguvu na matarajio ya ECOWAS inayojiandaa kupunguza au kuiondolea vikwazo Niger, ambavyo ni pamoja na kusimamisha uanachama wake kwenye soko la fedha la kikanda na Benki Kuu.