ECOWAS yawapa watawala wa kijeshi muda wa mwisho kuamua
17 Desemba 2024Uamuzi huo dhidi ya serikali za BurkinaFaso, Mali na Niger umekuja baada ya mataifa hayo matatu kusema maamuzi yao ya kujitowa kwenye jumuiya ya ECOWAS hayawezi kubadilishwa.
Soma pia: Viongozi wa ECOWAS wakutana kwenye mkutano wa kilele, katikati ya kitisho cha wengine kujitoa
Watawala wa mataifa hayo wanaishutumu jumuiya hiyo kuwa ni kibaraka cha wakoloni wao wa zamani Ufaransa. Kujiondowa kwa mataifa hayo katika jumuiya hiyo ya kikanda ni hatua inayoweza kusababisha athari kubwa katika biashara huria na usafiri pamoja na ushirikiano wa kiusalama.
Viongozi waliokutana kwenye mkutano wa kilele mjini Abuja, Nigeria pia walipitisha uamuzi wa wa kuundwa mahakama maalum itakayosikiliza kesi dhidi ya rais wa zamani wa Gambia,Yahya Jammeh, kutokana na uhalifu uliofanyika wakati wa utawala wake nchini humo.