EL-GENEINA : Wanamgambo wauwa ovyo Dafur
26 Aprili 2007Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika huko Dafur ya Magharibi kimeuambia Umoja wa Mataifa hapo jana kwamba wanamgambo wa Kiarabu wamekuwa wakiuwa na kupora katika jimbo hilo bila ya hofu ya kukamatwa na serikali ya Sudan.
Meja Harry Soko afisa wa Rwanda akimuarifu hayo mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa amesema kuwepo kwa makundi ya waasi wa Sudan katika eneo lao pia kumepelekea kuzuka kwa mizozo na mamia ya vifo katika miezi iliopita.
Amemuambia mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa Antonio Gueteres ambaye yuko ziarani katika jimbo la Dafur kwamba wanamgabo wa Kiarabu inaoaminika kuwa wameajiriwa na serikali ya Sudan wanatamba kwa uhuru katika eneo lilioko chini ya mamlaka yao na kumtishia na kumuuwa yoyote yule alie dhidi ya maslahi ya serikali.