Bunge la Uturuki lapokea ombi la Sweden kujiunga NATO
23 Oktoba 2023Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amewasilisha rasmi ombi la Sweden la kujiunga na Jumuiya ya kujihami, NATO kwenye bunge la nchini humo, hatua ambayo huenda ikahitimisha mvutano uliodumu kwa miezi 17 baina ya mataifa hayo.
Ofisi ya Erdogan imeandika kwenye ukurasa wake wa X, kwamba itifaki hiyo imesainiwa na rais Erdogan hii leo na kupelekwa kwenye Bunge la Kuu la Kitaifa la Uturuki.
Soma pia:Sweden yamtia hatiani mtuhumiwa wa kwanza wa kuchoma Quran
Erdogan amekuwa akichelewesha kuidhinisha itifaki hiyo akiituhumu Stockholm kwa kutokuwa na msimamo mkali dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi na makundi mengine inayoyaona kuwa kitisho cha usalama.
Wanachama wote 31 wa NATO wanatakiwa kuidhinisha uanachama wa Sweden, lakini Uturuki na Hungary bado hawajaidhinisha.