1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan hajaondoa uwezakano wa kurudisha uhusiano na Syria

28 Juni 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema hajaondoa uwezekano wa kukutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad kama sehemu ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4heHu
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Europa Press/ABACA/IMAGO

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema hajaondoa uwezekano wa kukutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad kama sehemu ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kauli iliyotolewa na Assad kwamba serikali yake imefungua milango ya kurejesha uhusiano na Uturuki alimradi Ankara itaheshimu uhuru wa Syria na kuchangia juhudi za kupambana na ugaidi, Erdogan amesema hakuna sababu ya kuzuia hilo kufanyika.Uturuki yashambulia ngome za Wakurdi nchini Syria na Iraq

Kiongozi huyo wa Uturuki ameongeza kuwa nchi yake haina nia ya kuingilia kati masuala ya ndani ya Syria.

Uturuki ilikata uhusiano wake na Syria mwaka 2011 baada ya kuibuka vita nchini Syria huku utawala wa Ankara ukiwaunga mkono waasi waliotaka kumuondoa Assad madarakani.