1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yaendelea kuzima mitandao

Daniel Gakuba
7 Juni 2017

Watumiaji wa mitandao ya kijamii kupitia simu za mkononi nchini Ethiopia bado hawapati huduma hiyo, licha ya madai ya serikali kwamba matatizo hayo ya kimtandao yaliyoanza wiki iliyopita yameondolewa.

https://p.dw.com/p/2eF33
Messenger-Dienste
Picha: picture-alliance/dpa/W. Kastl

Ethiopia, ambayo ni ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya wakazi barani Afrika, ilikata ghafla huduma ya mtandao wa mashirika hayo nchini kote bila onyo lolote, hali ambayo iliyaathiri pia majengo ya kidiplomasia kama lile la Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika, na makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Baadaye huduma katika majengo hayo ilirejeshwa, pamoja na ile inayotolewa kupitia njia ya Bradband, lakini wale huduma ya mtandao wa simu za mkononi, inayotumiwa na watu wengi na pia biashara, ilikuwa bado haipatikani.

Waziri wa Mawasiliano, Negeri Lencho, alisema huduma hiyo iliondolewa kwa muda ili kuwawezesha wanafunzi kujikita katika masomo yao wakati mtihani ukikaribia.