1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaUganda

EU kuekeza zaidi ya dola milioni 60 kwa umeme Uganda

30 Oktoba 2023

Umoja wa Ulaya unapanga kuekeza dola milioni 63 katika kuboresha mmojawapo ya mitambo mikubwa zaidi ya kufua umeme nchini Uganda.

https://p.dw.com/p/4YCE7
Miundombinu ya nishati ya Uganda inafadhiliwa kidogo na imezeeka, ikiwa ni hali ambayo husababisha kukatika kwa umeme mara kwa mara miongoni mwa sababu nyinginezo.
Miundombinu ya nishati ya Uganda inafadhiliwa kidogo na imezeeka, ikiwa ni hali ambayo husababisha kukatika kwa umeme mara kwa mara miongoni mwa sababu nyinginezo.Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP/Getty Images

Haya yamesemwa Jumatatu na Jan Sadek, balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Uganda.

Sadek amesema fedha hizo zitatumika kurekebisha viwanda vya Kiira na Nalubaale kwa ajili ya umeme utrakaosaidia katika kuiendeleza Uganda kiviwanda.

Balozi huyo lakini hakutoa tarehe kamili ya ufadhili huo na vile vile hakuweka wazi iwapo fedha hizo zitakuwa ni za mkopo.

Viwanda vya Nalubaale na Kiira vilivyo katika chanzo cha Mto Nile huko Jinja, vinazalisha megawati 380 za umeme na ndivyo viwanda vya zamani zaidi vya umeme nchini Uganda.