1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU kupeleka kitita cha msaada wa kiutu Lebanon

3 Oktoba 2024

Umoja wa Ulaya hii leo umesema utaipa Lebanon msaada zaidi wa Euro milioni 30 huku nchi hiyo ikiwa inakabiliwa na mapigano makali kati yake na Israel.

https://p.dw.com/p/4lN5N
Umoja wa Ulaya |  Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Dwi Anoraganingrum/Panama/IMAGO

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema msaada huo mpya wa fedha utahakikisha kuwa raia wa Lebabon wanapata misaada inayohitajika wakati huu wanapopitia wakati mgumu.

Soma pia:Mfuko wa dharura wa EU washindwa kuhudumia wahamiaji
Rais huyo wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuongezeka kwa mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati.  Amezitaka pande zote zinazopigana zihakikishe zinalinda maisha ya raia wasio na hatia.

Umoja wa Ulaya umetoa msaada wa fedha kwa Lebanon wa zaidi ya euro milioni 100 katika mwaka huu.