1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yaelekea kuisadia Iraq

Admin.WagnerD15 Agosti 2014

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wamekuwa na mwelekeo wa kuunga mkono jeshi la Kikurd katika kukabiliana na wapiganaji wenye kupigana vita vya Jihad- Dola la Kiislamu nchini Iraq.

https://p.dw.com/p/1CvX9
EU-Außenministertreffen in Brüssel 22.07.2014
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa UlayaPicha: picture-alliance/dpa

Katika mkutano huo wa mjini Brussels, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Laurent Fabius ameonekana kuwa kinara kwa kutoa wito kwa bara la Ulaya wa kujiunga pamoja na kufanikisha mpango wa kuwasaidia Wairaq na Wakurdi. Uingereza nayo inaonekana iko tayari kuzingantia pendekezo lolote la kusaidia kupeleka silaha.

Waziri wa Mambo ya Nje Philip Hammond alisema huwezi kufumba macho na kuwa mtazamaji katika kadhia hiyo. Aliongeza kusema inawezekana kwa hivi sasa maelfu ya Wairaq wanalazimisha kuyahama makazi yao au wanapoteza maisha yao kwa namna rahisi kabisa kwa sababu ya kuwa na mtazamo tofauti au dini nyingine. Waziri wa mambo ya nje wa Luxembourg Asslborn Jean Asslborn alisema vitendo hivyo lazima visiamishwe mara moja.

Kauli ya Steinmier wa Ujerumani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmier amesema Umoja wa Ulaya umeridhia baadhi ya mataifa ya Umoja wa Ulaya kukubali ombi la Wakurdi la kupatiwa silaha.

Aussenministertreffen Brüssel Steinmeier
Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Ujerumani, Frank-Walter SteinmierPicha: Reuters

Jeshi la Ujerumani jana limeanza kusafirisha kwa njia ya anga kiasi cha tani 36 za misaada ya madawa,vyakula na mablanketi kwa jamii ya Wakurdi, kwenye mji wa Arbil. Wakati wa kuanza kwa zoezi hilo wazri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula Von Der Leyen alitoa kauli hii alisema "Kwa hakika huu ni mwanzo tu, na tufanya jitihada zaidi kupeleka misaada zaidi kwa kadri iwezekanavyo. Na pia tunafanyia kazi suala la vifaa kama kofia za kujikinga kichwa na fulana kama vitahitajika. Jambo hilo litatimia iia kwa ukamilifu katika siku zijazo. Hii ni hatua inayofuata tunayofanyia kazi"

Kazi ya kuunda serikali mpya yaanza iraq

Wakati hayo yakitendeka Waziri Mkuu mteule wa Iraq, Haida al-Abadi jana alianza kuendesha mazungumzo ya kuunda serikali mpya. Mkutano huu wa dharura wa mawaziri wa mambo ya Nje unaondelea mjini Brussels unatarajiwa kutoa ahadi kuunga mkono kisiasa Iraq na mamlaka ya Kikurd.

Dola la Kiislamu, kundi la wenye msimamo mkali, limweza kuyadhibiti maeneo kadhaa nchini Iraq na Syria katika wiki za hivi karibu limeondosha maelfu ya watu kutoka jamii ya wachache ya Wayazidi na Wakristo katika makazi yao na kuweza pia kulishinda nguvu jeshi la Wakurdi.

Mwandishi: Sudi Mnette/DPA
Mhariri:Yusuf Saumu