F1: Leclerc aibuka mshindi wa mkondo wa Australia
11 Aprili 2022Na katika mbio za magari ya Formula One, baada ya kupata ushindi muhimu wa timu yake ya Ferrari katika mbio za Grand Prix za Australia jana Jumapili, imani ya dereva Charles Leclerc katika matarajio ya timu hiyo inaendelea kuwa kubwa kila baada ya mashindano. Mbio ambazo zilitarajiwa kuwa kati ya Ferrari ya Leclerc na Red Bull za Max Verstappen na Sergio Perez zilikamilika kwa faida ya Leclerc. Na sasa dereva huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Monaco ameongeza pengo la pointi zake za ubingwa wa dunia hadi 34 baada ya kupata ushindi wake wa pili msimu huu baada ya kushinda mbio za ufunguzi za mkondo wa Bahrain "Inapendeza zaidi.
Nina furaha kwa sababu Melbourne ni mkondo ambao nimekuwa nikipata matatizo sana katika siku za nyuma. Nimekuwa hapa mara mbili tu hapo kanla kwa sababu ulipfutwa kutona na covid, lakini sio mkondo ambao unanipa matokeo mazuri sana na nimekuwa nikijitahidi. katika kufuzu niliyaweka mambo sawa na katika mbio zenyewe nikaendesha gari jinsi tu nilivyotaka kuendesha.
Hitilafu ya injini ilimlazimu bingwa mtetezi Verstappen kujiondoa wakati akiwa kwenye mzunguko wa 38 wa mbio hizo. "Tunahitaji kuelewa kwa nini hali hiyo inatokea, kwa sababu kila mara tulipojaribu kumufuata Charles nilishindwa kabisa kumkaribia bila ya kuharibu matairi ya gari langu kwa hiyo nilijaribu tu kujiwekea mwendo wangu ukilinganisha na madereva waliokuwa nyuma. Tungeweza kupata nafasi ya pili lakini unapaswa kumaliza mbio ili upate nafasi ya pili hata kama mambo yanakuendea mrama. Hatufanyi hilo na bila shaka inasikitisha.
Mwenzake wa Redbull Perez alimaliza wa pili mbele ya madereva wa Mercedes George Russell na Lewis Hamilton katika nafasi ya tatu nan ne mfululizo. Madereva wa McLaren Lando Norris na Daniel Ricciardo walimaliza wa tano na sita.
afp, ap, reuters, dpa